Tanzania yapiga hatua katika kulinda na kutetea haki za binadamu, Makamu wa Rais afunguka Arusha.
Makamu
wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan, amesema, Serikali ya Tanzania
imepiga hatua kubwa katika kulinda na kutetea haki za binadamu kwa
kuzingatia maazimio mbalimbali ya ndani ya nchi na ya kimataifa ikiwemo
haki ya kuishi.
Mh.
Samia ametoa kauli hiyo jana jijini Arusha kwa niaba ya Rais Dk John
Pombe Magufuli wakati anafungua mkutano wa mazungumzo wa masuala ya
demokrasia na haki za binadamu ya Mahakama ya Afrika ya Watu na Haki za
binadamu.
Alisema
Tanzania ni mfano wa kuigwa barani Afrika kwa kuzingatia na kutekeleza
ipasavyo mikataba mbalimbali ya kimataifa inayolenga kuhakikisha
wananchi wake wanapata huduma bora na za msingi ikiwemo huduma ya afya
na elimu bila kubaguliwa kutokana na ulemavu,jinsia,rangi au dini.
Alisisitiza
kuwa Serikali itaendelea kutekeleza na kuzingatia matamko mbalimbali ya
Dunia yanayolenga kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za kijamii
ikiwemo haki ya kuishi.
Kwa upande wake, Rais wa Mahakama ya Afrika ya Watu na Haki za Binadamu Justice Sylvain Ore alisema
kuwa mkutano huo ni muhimu kwani unalenga kujadili na kuweka mikakati
inayolenga kuhakikisha nchi za Afrika zinazingatia na kulinda haki za
bindamu hasa haki za wanawake kwa kiwango kikubwa.
Mkutano
huo wa Mahakama ya Afrika ya Watu na Haki za Binadamu ambao unafanyika
Jijini Arusha umehudhuriwa na wajumbe kutoka mataifa mbalimbali ya
Afrika wakiwemo wajumbe kutoka Umoja wa Afrika AU na lengo la mkutano
huo ni kutajadili masuala ya demokrasia na haki za binadamu katika nchi
za Afrika.
Tanzania yapiga hatua katika kulinda na kutetea haki za binadamu, Makamu wa Rais afunguka Arusha.
Reviewed by bloger
on
November 23, 2016
Rating:
No comments