Adakwa akimfanyia mwanafunzi mtihani wa Form IV

Adakwa akimfanyia mwanafunzi mtihani wa Form IV
Jeshi la Polisi Zanzibar limemfukuza kazi askari wake baada ya kukamatwa akimfanyia mtihani mwanafunzi wa kidato cha nne kinyume na sheria huku kukiwa na taarifa za baadhi ya wanafunzi kukamatwa kwa kuhusika na kukutwa na mitihani ya kidato cha nne.

Kamanda wa Polisi wa mkoa wa mjini Magharibi kamishna msaidizi mwandamizi SACP Hassan Nassir amethibitisha kwa jeshi la polisi kumfukuza kazi askari huyo F9592 Hassan Haji Jecha ambaye kwa sasa ni mwanafunzi wa chuo kikuu akichuka digrii ya pili amekutwa akimfanyia mtihani mwanafunzi Said Haji kitendo ambacho ni aibu.

Katika hatua nyingine kundi kubwa la wazee walijazana nje ya makao makuu ya polisi mkoa wa mjini Magharibi wakilalamika watoto wao kuwekwa ndani bila ya taarifa kwa madai ya kuvujisha mitihani ya kidato cha nne kupitia mitandao ya simu.

Kulingana na kituo cha televisheni chaITV, baadhi ya wazee wa watoto hao wameshangazwa na uamuzi wa polisi kutotoa taarifa yeyote.

Wanafunzi hao idadi yao haijajulikana wamekamatwa kutoka sehemu mbalimbali huku pakiwa na taarifa ya baadhi ya wataalam kutoka Dar es Salaam wamewasili Zanzibar kufuatia suala hilo.

Hata hivyo wakati wazee hao wanawalilia watoto wao wakiwa ndani ya jengo la polisi kamanda Hassan Nassiri amepinga madai hayo akidai hana taarifa za kuwepo kwa tatizo hilo la kukamatwa wanafunzi kwa shutuma za mitihani hiyo ya kidato cha nne.
Adakwa akimfanyia mwanafunzi mtihani wa Form IV Adakwa akimfanyia mwanafunzi mtihani wa Form IV Reviewed by bloger on November 16, 2016 Rating: 5

No comments

Business

Post Navigation Display