Mikoa Mitano inayoongoza kwa Ndoa za utotoni Tanzania

Tanzania imetajwa kuwa ni moja kati ya nchi zenye viwango vya juu vya matukio ya ndoa za utotoni. Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) katika utafiti uliochapishwa mnamo Januari, 2016 uliitaja kuwa ni nchi ya tatu barani Afrika kwa matukio ya ndoa na mimba za utotoni kwa 28%.

Kutokana na shirika la Idadi ya Watu Duniani (UNFPA), kwa wastani watoto wakike wawili kati ya watano huolewa kabla ya kufikisha umri wa miaka 18. Pia takwimu za utafiti wa Idadi ya watu na Afya Tanzania (TDHS, 2010) 37% ya watoto wa kike Tanzania huolewa kabla ya kufikisha miaka 18.

Takwimu za shirika la Watoto Duniani (UNICEF 2012) lilitaja mikoa inayoongoza kwa ndoa za utotoni huku mkoa wa Shinyanga ukiongoza kwa 59%, ukifuatiwa na Tabora 58%, Mara 55%, Dodoma 51%, Lindi 48%.

Mikoa mingine inayofatia ni pamoja na Mbeya 45%, Morogoro 42%, Singida 42%, Rukwa 40%, Ruvuma 39%, Mwanza 37%, Kagera 36%, Mtwara 35%, Manyara 34%, Pwani 33%, Tanga 29%, Arusha 27%, Kilimanjaro 27%, Kigoma 26%, Dar es Salaam 19% na Iringa 8%.

Sababu kuu zinazochangia kukua kwa tatizo hili ni pamoja Mila na desturi potofu, Sheria na sera kinzani, Mifumo dhaifu ya uongozi katika ngazi ya kata, vijiji, Mitaa na vitongoji.
Mikoa Mitano inayoongoza kwa Ndoa za utotoni Tanzania Mikoa Mitano inayoongoza kwa Ndoa za utotoni Tanzania Reviewed by bloger on November 23, 2016 Rating: 5

No comments

Business

Post Navigation Display