PICHA: Mwanamke aliyekaa siku nzima kwenye Jeneza ili kupata uzoefu wa kifo.

Imetokea Brazil na Mwanamke mwenyewe anaitwa Vera Lucia da Silva na umri wake ni miaka 44 ambapo aliamua kukaa kwenye jeneza siku nzima ili apate uzoefu wa mazingira ya kifo ili siku akifa asiwe mgeni na Jeneza. 
image
Vera aliamua kukaa kwenye jeneza huku familia yake ikifanya vitu vinayofanywa kwenye msiba ili aone inakuaje ambapo baada ya kutoka humo alisema ilikua siku nzuri zaidi kwenye maisha yake yote.
Sherehe hiyo ya kujifunza maisha ya kwenye Jeneza ambayo ilifanyika Jumatano ya November 2 2016 ni sherehe ambayo ilifanyika kwenye eneo la makaburi.
image
Ndugu zake walipingana sana na wazo lake lakini baadae waliamua kukubaliana naye na kuvaa nguo nyeusi wakati walipomtembelea na kufanya kama wanatoa heshima za mwisho.
image
Mmiliku wa eneo la kuzikia liitwalo Eternal Garden Funeral home, Paulo Araujo, aliamua kumpa Jeneza Vera bila gharama zozote, kama mgeni maalumu.
Wakati akiwa ndani ya Jeneza mwanamke huyo alikua akifumbua macho na kufumba kama vile mtu aliyekufa na kufufuka.
image
Mwanamke huyo amesema alikuwa na ndoto ya kulala kwenye Jeneza tangu miaka 14 iliyopita na hakuwa akifikiri ingekuja kutokea akaitimiza, kwasasa amefurahi kutimiza alichokitaka kabla hajafa.
PICHA: Mwanamke aliyekaa siku nzima kwenye Jeneza ili kupata uzoefu wa kifo. PICHA: Mwanamke aliyekaa siku nzima kwenye Jeneza ili kupata uzoefu wa kifo. Reviewed by bloger on November 04, 2016 Rating: 5

No comments

Business

Post Navigation Display