SERIKALI MBIONI KUVIFUTA VYUO VIKUU ‘UCHWARA’


Serikali imebaini kuwepo kwa vyuo vikuu vingi visivyo na sifa, hivyo inakusudia kuvifuta lengo likiwa ni kuhakikisha inaimarisha kiwango cha elimu inayotolewa kwa ngazi zote.

Waziri wa Elimu, Profesa Joyce  Ndalichako ameyasema hayo  , wakati akifungua  mkutano wa siku mbili wa  wadau wa elimu ya juu.

Amesema hayo yamebainika baada ya jopo la wataalamu kufanya uhakiki kwenye vyuo hivyo nchini.ndalichako

“Lengo ni kuhakikisha wasomi wanaohitimu kwenye vyuo hivyo wanakuwa wameiva kitaaluma, ili pia waweze kushiriki katika kuijenga Tanzania ya viwanda,” amesema  Profesa Ndalichako.

Mwenyekiti wa Bodi ya Tume ya vyuo vikuu nchini(TCU) Profesa Jacob Mtabaji amesema  wamejipanga kuhakikisha kwamba wanafanyakazi zao kwa kusimamia mwongozo uliopo ili kuondoa uwepo wa vyuo vingi visivyo na sifa

SERIKALI MBIONI KUVIFUTA VYUO VIKUU ‘UCHWARA’ SERIKALI MBIONI KUVIFUTA VYUO VIKUU ‘UCHWARA’ Reviewed by bloger on November 21, 2016 Rating: 5

No comments

Business

Post Navigation Display