Mkwassa atangaza kikosi cha Stars

Mkwassa atangaza kikosi cha Stars



    Kocha wa Taifa Stars, Charles Boniface Mkwassa ametangaza kikosi chake kitakachoivaa Zimbabwe katika mechi ya kirafiki.

    Mkwasa amewachota viungo wapya ambao wengi wao walionekana hawana nafasi awali.

    Mkwasa ameita jumla ya nyota 24 ambao watasafiri kuifuata Zimbabwe Novemba 12, mwaka huu ikiwa ni siku moja kabla ya mchezo huo ulio kwenye kalenda ya Fifa.

    Aidha, Mkwassa ameingiza sura mpya kama, fowadi Omary Mponda wa Ndanda, kipa Said Kipao na beki Aidan Michael (JKT) na beki James Josephat wa Prisons na kuwatema masta kama Deus Kaseke, Kelvin Yondani, Hassan Kessy (Yanga), Mwinyi Kazimoto (Simba), Salum Aboubakar, Aggrey Morris (Azam).

    Akitangaza kikosi hicho, Msemaji wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Alfred Lucas alisema: “Kikosi kitaingia kambini siku moja baada ya raundi ya kwanza kumalizika, yaani Novemba 7 mpaka Novemba 11 kabla ya kusafiri kesho yake kuifuata Zimbabwe.”

    MAKIPA:
    Aishi Manula (Azam), deugratius Munishi (Yanga) na Kipao (JKT Ruvu).

    MABEKI:
    Erasto Nyoni, David Mwantika (Azam), Michael (JKT), Vicent Andrew, Haji Mwinyi (Yanga) na Josephat (Prisons).

    VIUNGO:
    Jonas Mkude, Shiza Kichuya, Mohammed Ibrahim ‘Cabaye’, Jamal Mnyate na Yassin Mzamiru (wote Simba) Himid Mao (Azam) na Abdulrahman Mussa (Ruvu Shooting).

    WASHAMBULIAJI:
    John Bocco (Azam), Ibrahim Ajibu (Simba), Mbwana Samatta (KRC Genk, Ubelgiji), Elias Maguri (Dhofar, Oman), Thomas Ulimwengu (huru) na Omary Mponda wa Ndanda.

    Lucas alisema kutokana na mbanano wa michezo, mechi za viporo Simba vs Prisons, Yanga vs Ruvu Shooting na Mwadui vs Azam, zote zimepangwa kupigwa Novemba 10.
Mkwassa atangaza kikosi cha Stars Mkwassa atangaza kikosi cha Stars Reviewed by bloger on November 04, 2016 Rating: 5

No comments

Business

Post Navigation Display