MAHAKAMA YA MAFISADI YAANZA KAZI KWA KUDAI FIDIA YA MABILIONI

Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, maarufu Mahakama ya Mafisadi imewapa masharti sita ya dhamana washtakiwa wa kesi ya uhujumu uchumi wanaodaiwa   kukutwa na nyavu haramu za kuvulia samaki katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Katika masharti hayo, Mahakama imemtaka mshtakiwa Ally Raza (34) kuwasilisha mahakamani fedha taslimu Sh2,582,191,666 (zaidi ya Sh2.5 bilioni), au hati ya mali yenye thamani sawa na kiasi hicho.

Mshtakiwa Jeremiah Kerenge (40), ametakiwa kuwasilisha mahakamani Sh4,454,241,666 (zaidi ya Sh4.4 bilioni), au hati ya mali yenye thamani sawa na kiasi hicho.

MAHAKAMA YA MAFISADI YAANZA KAZI KWA KUDAI FIDIA YA MABILIONI MAHAKAMA YA MAFISADI YAANZA KAZI KWA KUDAI FIDIA YA MABILIONI Reviewed by bloger on November 16, 2016 Rating: 5

No comments

Business

Post Navigation Display