Waziri Mkuu wa zamani Israel afariki dunia

Waziri Mkuu wa zamani Israel afariki dunia


  • Waziri mkuu na rais wa zamani wa Israel Shimon Peres amefariki dunia mapema leo akiwa na umri wa miaka 93 baada ya kuugua kiharusi, wiki mbili zilizopita.

  • Mshindi huyo wa tuzo ya amani ya Nobel alikimbizwa hospitalini Tel Aviv wiki mbili zilizopita baada ya kuugua kiharusi ghafla.

    Kutokana na msiba huo, Rais wa Marekani Barack Obama ametuma salama za rambirambi kwa serikali ya Israel.

    “Kuna watu wachache duniani ambao wamethubutu kubadili historia ya binadamu, si kwa kupitia majukumu yao kama binadamu, ni kwa sababu ya kutanua fikra za uadilifu na kutufanya tufikiri makubwa kutoka kwetu sisi wenyewe,” Rais Obama amesema kupitia taarifa ya White House iliyotolewa mapema leo.

    Ofisi ya Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, anayetarajiwa kutoa hotuba muda si mrefu imetuma salamu za rambirambi kwa familia ya Peres.

    “Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu na mke wake Sara wanaeleza masikitiko yao kwa kifo cha mpendwa rais wa zamani wa Israel, Shimon Peres,” inasema sehemu ya taarifa ya Netanyahu.
Waziri Mkuu wa zamani Israel afariki dunia Waziri Mkuu wa zamani Israel afariki dunia Reviewed by bloger on September 28, 2016 Rating: 5

No comments

Business

Post Navigation Display