Aua mwanawe kisha ajiua

Aua mwanawe kisha ajiua

  • posted about 1h ago
  •  
  • 27-09-2016 10:54
  •  
  • Kitaifa
  • Mwinjilisti wa Kanisa la African Inland Church (AICT), Charles Kazereng'wa (45), amejinyonga hadi kufa, baada ya kumuua mwanaye, Malita Charles (15) kwa kumpiga akimtuhumu kujihusisha na ufuska.

    Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Geita, Mponjoli Rodson amelithibitishia gazeti hili kutokea kwa matukio hayo juzi jioni.

    Hata hivyo, alisema kuwa asingeweza kulizungumzia suala hilo kwa undani kwa sababu alikuwa kwenye sherehe za uzinduzi wa Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani ambayo kitaifa inafanyika mkoani Geita.

    Hata hivyo, habari za uhakika kutoka katika Kitongoji cha Elimu, Kijiji cha Kaseme kilichopo wilayani Geita ambako mwinjilisti huyo alikuwa akiishi na familia yake zinasema kuwa alichukua uamuzi wa kumwadhibu binti yake huyo aliyehitimu darasa la saba mwaka huu, baada ya kumkuta akizungumza na mwanamume ambaye hata hivyo hakufahamika.

Aua mwanawe kisha ajiua Aua mwanawe kisha ajiua Reviewed by bloger on September 27, 2016 Rating: 5

No comments

Business

Post Navigation Display