Beki wa PSG ahukumiwa jela




Beki wa PSG ahukumiwa jela

  • posted about 12h 28m 1s ago
  •  
  • 26-09-2016 19:57
  •  
  • Michezo
  • Beki wa kulia wa Paris St Germain, Serge Aurier ambaye ni raia wa Ivory Coast amehukumiwa kwenda jela miezi miwili kutokana na kukutwa na kosa la kumfanyia fujo askari polisi nchini Ufarasa.

    Beki huyo mwenye umri wa miaka 23 alifanya kosa hilo jijini Paris, Mei 30, mwaka huu ambapo inaelezwa alimshambulia na kumtolea maneno makali.

    Mbali na adhabu hiyo pia amepigwa faini ya euro 600 na mahakama na zinaweza kuongezeka euro 1,500.

    Mwanasheria wa mchezaji huyo amesema atakata rufaa kupinga adhabu hiyo, lakini bado kanuni zinamruhusu kuibadili na kuifanya kuwa adhabu ya kuitumikia jamii badala ya kwenda jela.

    Pia mchezaji huyo anatarajiwa kuwemo katika kikosi cha PSG kitakachocheza keshokutwa Jumatano katika Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Ludogorets.

    Mpaka sasa ameshaichezea PSG mechi 5 msimu huu na kutoa asisti kwa Edinson Cavani katika mechi dhidi ya Arsenal, wiki mbili zilizopita.
Beki wa PSG ahukumiwa jela Beki wa PSG ahukumiwa jela Reviewed by bloger on September 27, 2016 Rating: 5

No comments

Business

Post Navigation Display