Baada ya kuzushiwa kifo, Bilionea Dangote ameyaandika haya


Bilionea namba moja barani Afrika, Aliko Dangote amekanusha uvumi unaosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa amefariki dunia akiwa nchini Ujerumani.

Taarifa hizo zinaeleza kuwa bilionea huyo amefariki akiwa nchini Ujerumani baada ya kuugua kwa muda mfupi. Aidha, taarifa hizo zinaeleza kuwa familia ya bilionea huyo imethibitisha kifo cha ndugu yao huyo na kusema kuwa ni pigo kubwa kwa Afrika.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Dangote ameandika hivi “I am hale, hearty and alive. Please disregard malicious report saying otherwise. Thank you.” , akimaanisha kuwa yeye ni mzima wa afya na kuwataka watu kupuuzia taarifa zinazoeleza kivingine.”

<<<SOMA ZAIDI HAPA>>>
Baada ya kuzushiwa kifo, Bilionea Dangote ameyaandika haya Baada ya kuzushiwa kifo, Bilionea Dangote ameyaandika haya Reviewed by bloger on September 27, 2016 Rating: 5

No comments

Business

Post Navigation Display