RIPOTI ya Benki ya Dunia kuhusu Uchumi wa Tanzania na Rwanda iko hapa..


Mtu wangu nakusogezea tena taarifa hii kutoka Benki ya Dunia ambayo imetoa ripoti ya ustawi wa uchumi wa Afrika ambapo nchi za Afrika Mashariki za Tanzania na Rwanda zinaonekana kuwa na uchumi wenye kustawi kwa wastani.
Ripoti mpya ya Benki ya dunia itolewayo mara mbili kwa mwaka, Africa’s Pulse, inaonesha kuwa mwelekeo wa ukuaji uchumi barani Afrika unatarajiwa kudorora zaidi na kuwa asilimia moja nukta sita mwaka huu ikilinganishwa na asilimia tatu mwaka jana.
Hata hivyo imebainisha kuwa, mwelekeo wa ukuaji unatofautiana ambapo baadhi ya nchi ustawi umedorora huku nyingine uchumi unakua. Kwa mfano Rwanda, Tanzania na Ethiopia zimetajwa kuwa nchi zenye ustawi wa wastani ambao ni zaidi ya asilimia sita kwa mwaka, huku Cote d’Ivoire na Senegal zikiongoza kwa kasi ya ustawi barani Afrika.
Mchumi Mkuu wa Benki ya dunia kuhusu Afrika Albert Zeufack amesema chanzo cha kukwama ustawi wa uchumi ni kudorora kwa bei za bidhaa ikiwemo mafuta, hali ngumu ya kifedha na sera za uchumi zisizo makini.
Benki ya Dunia inasema mwelekeo ni kupanua wigo wa bidhaa zinazouzwa pamoja na kuboresha sekta ya kilimo hasa kwa wakulima wadogo wadogo ili kuinua vipato vyao na kupunguza umaskini.
RIPOTI ya Benki ya Dunia kuhusu Uchumi wa Tanzania na Rwanda iko hapa.. RIPOTI ya Benki ya Dunia kuhusu Uchumi wa Tanzania na Rwanda iko hapa.. Reviewed by bloger on September 30, 2016 Rating: 5

No comments

Business

Post Navigation Display