Waliofungua akaunti feki wapandishwa kizimbani

Waliofungua akaunti feki wapandishwa kizimbani


  • Watumishi watatu wa serikali na Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Bukoba mjini jana walipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Bukoba kusomewa mashitaka mawili likiwemo la kutaka kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

  • Washitakiwa hao wanadaiwa kufungua akaunti feki ya KAMATI MAAFA KAGERA kwa ajili ya kupokea misaada ya kifedha kwa waathirika wa tetemeko la ardhi lililotokea Septemba 10, mwaka huu.

    Watumishi waliofikishwa mahakamani hapo katika kesi hiyo namba 239/2016 ni aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera, Amantius Msole, Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Bukoba, Kelvin Makonda, Mhasibu wa Mkoa wa Kagera, Simbaufoo Swai na Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Bukoba, Carlos Sendwa.

    Wakili wa Serikali, Hashimu Ngole amedai mahakamani kuwa, wanashitakiwa kwa makosa mawili likiwemo la kula njama za kutenda kosa kufungua akaunti feki yenye jina linalofanana na jina la akaunti ya KAMATI MAAFA KAGERA yenye namba 015225617300 ambayo wao walifungua akaunti yenye jina la KAMATI MAAFA KAGERA yenye namba 0150225617300.

    Alilitaja shitaka la pili ni kutumia madaraka na vyeo vyao vibaya kinyume cha sheria.

    Mawakili wanaowatetea watuhumiwa hao walimwomba hakimu awapatie dhamana wateja wao kwakuwa bado ni watumishi wa serikali na wanao uwezo wa kujidhamini wenyewe na hawawezi kutoka nje ya Kagera.

    Hakimu Mkazi wa mahakama hiyo, Denis Mpelembwa aliahirisha kesi hiyo hadi leo ili kupitia upya vifungu vya sheria na kujiridhisha kama watuhumiwa wanastahili.
Waliofungua akaunti feki wapandishwa kizimbani Waliofungua akaunti feki wapandishwa kizimbani Reviewed by bloger on September 30, 2016 Rating: 5

No comments

Business

Post Navigation Display