Wabunge EU wamuunga mkono Magufuli

Wabunge EU wamuunga mkono Magufuli

  • posted about 1h ago
  •  
  • 27-09-2016 10:50
  •  
  • Kitaifa
  • Wakati Rais John Magufuli wa Tanzania akishikilia msimamo kuwa nchi yake haitasaini Mkataba wa Ushirikiano wa Kiuchumi (EPA) na Umoja wa Ulaya (EU) mpaka dosari kadhaa zitakaporekebishwa, baadhi ya wabunge wa EU wamemuunga mkono na kutahadharisha mkataba wa sasa utaua viwanda vya ndani.

    Siku kadhaa zilizopita, msimamo wa Tanzania na Burundi ulilazimisha nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), kukubaliana kusogeza mbele makubaliano ya ama zote zisaini mkataba huo au la ili kuruhusu uchambuzi zaidi.

    Tayari nchi za Kenya, Uganda na Rwanda zimekubaliana na mkataba huo wa EPA huku Tanzania na Burundi zikitoa sababu nzito za kiuchumi, zinazolenga kuhakikisha kuwa kabla ya kusaini mkataba huo, ni vyema suala la ulinzi wa viwanda vya ndani likazingatiwa.

    Mkataba huo unapaswa kusainiwa na nchi zote ili uanze kutumika katika ukanda mzima.

    Chini ya mkataba huo ambao majadiliano yake yalianza tangu mwaka 2007, EU inaahidi kuzipatia bidhaa kutoka ukanda wa Afrika Mashariki soko kwa kutotozwa kodi zinapopelekwa kwa nchi wanachama wa Ulaya, lakini na yenyewe italeta bidhaa zake katika soko la ukanda bila kutozwa kodi. Hata hivyo, msimamo wa Tanzania umesimama katika ulinzi wa viwanda vya ndani, hasa wakati huu Serikali ikijikita zaidi katika uchumi wa viwanda.

    Msimamo huo sasa unaungwa mkono na wabunge wawili wa EU, Marie Arena na Julie Ward, ambao wanashauri Afrika Mashariki isisaini mkataba huo wa ubia kwa namna ulivyo sasa.

    Katika mahojiano yao maalumu na mwandishi wa mtandao wa jarida mashuhuri la The New Times, wabunge hao wanasema bayana kuwa uamuzi wa Wakuu wa Nchi za Afrika Mashariki wa kuahirisha kusaini ubia huo hadi mwakani ili watafakari zaidi uko sahihi.

    “Tunaamini mkataba huu kwa namna ulivyo sasa hauko sawa. Ulaya inaitumia Kenya ambayo ndiyo yenye maslahi zaidi katika mkataba huu kuwa kama ngao yao. Wakati Kenya ilishaendelea kiviwanda, hali sio kama hivyo kwa Tanzania, Uganda na Burundi ambazo hazitafaidika
Wabunge EU wamuunga mkono Magufuli Wabunge EU wamuunga mkono Magufuli Reviewed by bloger on September 27, 2016 Rating: 5

No comments

Business

Post Navigation Display