Stand United yamvurugia Ngoma


Stand United yamvurugia Ngoma

  • posted about 1h ago
  •  
  • 27-09-2016 11:13
  •  
  • Michezo
  • Zikiwa zimebaki siku nne kabla ya mechi ya watani wa jadi, Simba na Yanga, rekodi ya kupachika mabao ya mshambuliaji anayetegemewa Jangwani, Donald Ngoma imetibuliwa na Stand United.

    Kipigo cha bao 1-0 kwenye Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga juzi, hakijaishia tu kufuta ndoto za Yanga kucherza mechi 19 za Ligi Kuu bila kupoteza, bali pia kimeharibu rekodi ya straika huyo wa kimataifa wa Zimbabwe kufunga katika kila mechi anayocheza kwenye Uwanja wa Kambarage.

    Tangu ajiunge na mabingwa hao wa kihistoria wa Tanzania Bara msimu uliopita akitokea FC Platinum ya kwao Zaimbabwe kwa dau linalotajwa kuwa Sh. milioni 97, Ngoma alifunga katika mechi zote tatu alizocheza kwenye uwanja huo wa Usukumani dhidi ya Stand United na Mwadui FC kabla ya juzi kutoka kapa.

    Kwa ujumla, straika huyo anayesifika kwa kuwa na nguvu nyingi, amefanikiwa kufunga mabao matano kwenye Uwanja wa Kambarage tangu atue nchini.

    Mechi yake ya kwanza ilikuwa Oktoba 28, mwaka jana alipofunga mabao yote mawili wakati kikosi cha Hans van der Pluijm kiliposhikwa kwa sare ya 2-2 na wenyeji Mwadui FC.

    Ngoma alifunga pia mabao mawili, Yanga iliposhinda 3-1 dhidi ya Stand United mjini Shinyanga msimu uliopita. Goli lingine la Yanga lilifungwa na Mrundi Amissi Tambwe.

    Nyota ya Mzimbabwe huyo iling'ara pia katika mechi yao ya kwanza Kanda ya Ziwa aliyofunga goli moja waliposhinda 2-0 dhidi ya Mwadui FC Septemba 17, mwaka huu.

    Wakati Ngoma akishindwa kung'ara kwa mara ya kwanza kwenye Uwanja wa Kambarage, mfungaji wa bao la juzi la Stand United, Pastori Athanas, ameweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kuifunga timu hiyo ya Jangwani msimu huu.

    Kabla ya mechi hiyo, Yanga ilikuwa imecheza mechi nne ikishinda tatu na kutoka sare mara moja.<<<SOMA ZAIDI>>>
Stand United yamvurugia Ngoma Stand United yamvurugia Ngoma Reviewed by bloger on September 27, 2016 Rating: 5

No comments

Business

Post Navigation Display