SAFARI ZA NDEGE KWA DAKIKA 8 KUZINDULIWA
Uswisi na Ujerumani ndio nchi pekee duniani zilizobahatika kuwa wa kwanza kuanzisha safari fupi zaidi za ndege ya kimataifa inayotarajiwa kuanza rasmi mwezi Novemba mwaka huu.
Safari hiyo fupi ya ndege itafanyika kati ya Uwanja wa ndege wa St. Gallen-Altenrhein nchini Uswisi na mji wa Friedrichshafen uliopo Mkoani Baden- Württemberg nchini Ujerumani.
Safari hiyo pia itatekelezwa kupitia mto Bodensee katika masafa ya umbali wa kilomita 21, moja kwa moja badala ya kilomita 62 kwa muda wa dakika 8 pekee.
Kulingana na taarifa iliyochapisha na Travelbook, safari hiyo ya ndege itaanzishwa Novemba 2 mwaka huu na Shirika la Ndege la People’s Viennaline kutoka Austria ambapo ndege zenye uwezo wa kubeba abiria 50 zitatumika siku mbili kwa wiki.
Safari ya ndege inalenga kusafirisha wafanyabiashara kati ya Altenrhein na Friedrichshafen na baadaye itafikia hadi Köln, huku tiketi za ndege zitauzwa kwa bei ya Euro 179 na safari moja ya kwenda pekee itagharimu Euro 40.
SAFARI ZA NDEGE KWA DAKIKA 8 KUZINDULIWA
Reviewed by bloger
on
September 27, 2016
Rating:
No comments