SAMWELI SITTA AENDA UJERUMANI KUTIBIWA

Aliyekuwa Spika wa Bunge, Samuel Sitta amekwenda Ujerumani kwa ajili ya matibabu ya miguu.

Mwanawe, Benjamin Sitta amesema: “Anachoumwa ni miguu. Baba yupo katika hali nzuri, yupo salama tu, achaneni na taarifa za mitandao.” Alikuwa akirejea taarifa zilizoenea kwenye mitandao kwamba baba yake yu mahututi.

Septemba 19, Rais John Magufuli alimtembelea Sitta nyumbani kwake ambako alimueleza kuwa hali yake inaendelea vizuri. Taarifa ya Ikulu ilieleza  mwanasiasa huyo mkongwe alikuwa jijini kwa ajili ya matibabu bila kueleza ugonjwa unaomsumbua.





SAMWELI SITTA AENDA UJERUMANI KUTIBIWA SAMWELI SITTA AENDA UJERUMANI KUTIBIWA Reviewed by bloger on September 28, 2016 Rating: 5

No comments

Business

Post Navigation Display