RAISI DOKT.SHEIKN AWAPA KILA MMOJA KIWANJA NA SH.MILIONI TATU WACHEZAJI WA ZANZIBAR HEROES



Raisi wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la mapinduzi Dkt. Ali Mohamedi Sheikn ametoa zawadi ya kiwanja kwa kila mchezaji wa Zanzibari Heroes na shilingi milioni tatu kwa kila mchezaji.

Dkt. Shein ametoa zawadi hizo katika hafla ya kuwapongeza wachezaji wa Zanzibar Heroes baada ya kufanya vizuri katika michuano ya ukanda wa Afrika Mashariki na Kati CECAFA.

"Mmeonyesha kwamba mnaweza soka katika michuano ya CECAFA, kama serikali inabidi tuwatunuku zawadi, jumla mko thelatini na tatu pamoja na wachezani na viongozi wa timu, kwa hiyo natoa pesa shilingi milioni tatu kwa kila mchezaji na viongozi wenu pamoja na kiwanja kwa kila mchezaji na nkiongozi na viwanja vyote vitakua sehemu moja mtaanzisha kijiji chenu" amesema Shein.

Zanzibar Heroes walimaliza katika nafasi ya pili katika michuano ya CECAFA huku wakiwa na rekedi nzuri baada ya kumtoa bingwa mtetezi UGANDA na kuwafunga ndugu zao KILIMANJARO STARS.

RAISI DOKT.SHEIKN AWAPA KILA MMOJA KIWANJA NA SH.MILIONI TATU WACHEZAJI WA ZANZIBAR HEROES RAISI DOKT.SHEIKN AWAPA KILA MMOJA KIWANJA NA SH.MILIONI TATU WACHEZAJI WA ZANZIBAR HEROES Reviewed by Joshua Mshana on December 24, 2017 Rating: 5

No comments

Business

Post Navigation Display